ZOEZI LA UFUATILIAJI WA MAENDELEO YA VIKUNDI VYA WAKULIMA WA MWANI

Shirika la LANGO limefanya ziara ya kukagua mashamba ya vikundi vya wakulima wa mwani katika Kata ya Mchinga Manispaa ya Lindi kwa lengo la kutathimini maendeleo ya shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo.

Kusudio kuu la LANGO ni kutaka kuona na kufahamu kwamba juhudi zinazofanywa na shirika hilo la kuwezesha na kuinua maisha ya wananchi wenye kipato cha chini kabisa kwamba zinaleta tija au la.

Hali tuliyoikuta inaleta matumaini makubwa kutokana na juhudi zinazowekwa na wakulima hao kwani wameshapanda mashamba yao wanasubiri tu wakati wa mavuno. Lakini pia vikundi hivyo vimeshaanza kutengeneza sabuni za maji kwa kutumia zao hilo la mwani na wako tayari kuzipeleka sokoni.

Bado kilio chao kikubwa kipo katika ukosefu wa wateja wa uhakika katika kata hiyo kulinganisha na maeneo mengine yanayolima zao la mwani. Wito wao kwa Serikali na wadau mbalimbali wa zao hilo ni kujitokeza ili kupata ufumbuzi wa changamoto za masoko ya uhakika.



Leave a Reply