UTAMBUZI WA WARAGHBISHI

Katika kuanza utekelezaji wa mradi wa Uraghbishi, LANGO kwa ufadhili wa shirika la TWAWEZA East Africa, limesimamia shughuli za kutambulisha mradi kwa wanajamii wa vijiji vinavyoguswa na mradi huo pamoja na kusimamia uchaguzi katika kila kijiji ili kupata wawakilishi wawili kutoka katika kila kijiji ambao watakwenda kupewa mafunzo ya dhana nzima ya Uraghbishi.

Zoezi hilo lilijengwa katika dhima ya ushiriki wa moja kwa moja kwa wanajamii wenyewe kufanya maamuzi ambapo upatikanaji wa waraghbishi hao ulifanyika kwa njia ya uchaguzi wa kura za wazi katika mikutano ya vijiji vyote kumi.

Kifuatacho sasa ni kwa wawakilishi hao kupewa elimu ya Uraghbishi itakayo wawezesha kupata ujuzi wa kutambua (kuibua), kuchambua na kutekeleza changamoto mbalimbali zilizopo na zitakazoibuka katika jamii zao kwa ufanisi zaidi ili kuleta maendeleo yenye tija.

Vijiji vitakavyoguswa na mradi huu ni pamoja na kijiji cha Sudi, Hingawari, Mandawa, Mmumbu, Mtualonga, Nahukahuka-B, Chihuta, Mtakuja, Mwangu na Namangale ambavyo vyote vipo katika halmashauri ya Mtama mkoani Lindi.

 

Wanajamii wa kijiji cha Hingawari wakiwa katika mkutano wa kijiji katika zozei la uchaguzi

 

Wanajamii wa kijiji cha Sudi wakiwa katika mutano wa kijiji kutekeleza zoezi la uchaguzi

 

Wanajamii wa kijiji cha Chihuta wakiwa kwenye mkutano wa kijiji kutekeleza zoezi la uchaguzi

 

Wanajamii wa kijiji cha Mwangu wakiwa katika mkutano wa kijiji kutekeleza zoezi la uchaguzi

 

Wanajamii wa kijiji cha Mtualonga wakiwa katika mkutano wa kijiji kutekeleza zoezi la uchaguzi
Wanajamii wa kijiji cha Nahukahuka-B wakiwa katika mkutano wa kijiji kutekeleza zoezi la uchaguzi
Wanajamii wa kijiji cha Namangale wakiwa katika mkutano wa kijiji kutekeleza zoezi la uchaguzi
Wanajamii wa kijiji cha Mtakuja wakiwa katika mkutano wa kijiji kutekeleza zoezi la uchaguzi

 Leave a Reply