ZIARA YA WAKULIMA WA MWANI LINDI NA MTWARA KWENDA ZANZIBAR

Wakulima wa zao la mwani kutoka Lindi na Mtwara wakifuatilia kwa makini mafunzo nadharia yaliyokua yakiendelea

Mkulima wa mwani kutoka Paje, Zanzibar akifundisha kwa vitendo jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji inayotokana na zao la mwani
Wakulima wa mwani kutoka Lindi na Mtwara wakijifunza jambo juu ya kilimo cha mwani katika mashamba ya mwani yanayomilikwa na ushirika huo

Wakulima wa mwani kutoka Lindi wakikagua mashamba ya mwani Zanzibar
Baadhi ya bidhaa zitokanazo na zao la mwani zinazozalishwa na ushirika huo
Wakulima wa mwani Lindi na Mtwara pamoja na wafanyakazi wa LANGO na MSOAPO wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ofisi za ushirika wa Furahia Wanawake Group Paje, Zanzibar

Katika kuendelea kutekeleza mradi wa Kuimarisha Usawa wa Kijinsia na Kuwezesha Kiuchumi Wanawake na Vijana kupitia zao la mwani, shirika la LANGO kwa udhamini wa shirika la Oxfam limeratibu ziara ya mafunzo kutoka Lindi kwenda Paje, Zanzibar katika kikundi cha Furahia Wanawake  Group. Ziara hiyo ya siku mbili iliyojumuisha wawakilishi wa vikundi vya wakulima wa mwani kutoka katika kata ya Mchinga, Manispaa ya Lindi, na kushirikiana na shirika la MSOAPO Mtwara ikijumuisha na wawakilishi wa wakulima katika mkoa huo.

Wakulima hao wa mikoa ya Lindi na Mtwara wamekutana na wakulima na wasindikaji wa zao la mwani wa Paje, Zanzibar kwa lengo la kuongeza ujuzi na ufanisi zaidi wa zao la mwani ili kuongeza tija kwa wakulima hao.

Wakulima waliweza kupata mafunzo ya nadharia na vitendo juu ya ulimaji, usindikaji, na utengenezaji wa bidhaa zinazotokana na zao hilo.

Ikumbukwe, kikundi cha Furahia Wanawake Group kilianza kilimo cha mwani mnamo 1990 wakiwa jumla ya wanachama 35, na sasa wapo jumla ya wanachama 29 wote wanawake ambapo mnamo 2011 waliamua kusajili umoja wao na kuunda Furahia Wanawake Group. Ushirika wao umefanikiwa kufanya vizuri katika kilimo hiko hata kuweza kuvutia serikali na kuifanya serikali kutoa kipaumbele kufanya kilimo cha mwani kama chanzo namba tatu cha kuongeza kipato na shughuli kuu ya kiuchiumi Zanzibar.

Si hivyo tu, mnamo tar. 03 Julai, 2021 raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dr. Mwinyi alitembelea kiwandani kwao kuokana na mafanikio ya ushirika huo. Kwa sasa kikundi kinajishughulisha na kulima mwani, kusindika, na kutengeneza bidhaa zinazotokana na mwani kama vile unga wa mwani, mafuta ya mgando, sabuni ya maji na sabuni ya miche.



Leave a Reply