UGAWAJI WA ZANA ZA KUZALISHIA ZAO LA MWANI

Shirika la LANGO kwa ufadhili wa shirika la OXFAM Tanzania limegawa zana za kuzalishia zao la mwani katika kata ya Mchinga Manispaa ya Lindi kwa lengo la kuboresha uzalishaji na kuwainua kiuchumi wakulima wa zao hilo.

Hii ikiwa ni mwendelezo wa shirika hilo kugawa zana za kilimo kwa makundi ya wakulima wa mwani ambao wanaonesha utayari na uthubutu wa kuzalisha zao hilo kwa kiwango kinacholeta tija.

Diwani wa kata hiyo Ndg. Mswalile Issa Ally amesema kwa juhudi hizi zilizofanywa na shirika la LANGO zimempa ari ya kusimamia kilimo hiko kwa ukaribu zaidi ili kuboresha uzalishaji. “Nitahakikisha mimi kama Diwani naingia mpaka baharini kwenyewe kuhakikisha hivi vifaa tulivyopewa vinafanyiwa kazi na kutuletea matokeo ambayo wote tunayatarajia na naamini mavuno yakiwa mazuri hata LANGO wenyewe watapata moyo wa kuendelea kutuinua katika pembejeo na mambo mengine. Kwa hiyo natoa rai kwa wakulima waliopokea vifaa hivi, wasiende kubweteka, bali wakafanye kazi kwa nguvu zao zote ili waweze kujikwamua kiuchumi”.

_MG_4862


Leave a Reply