- July 9, 2021
- Posted by: Lango Tanzania
- Category: Latest News
Wananchi wa Lindi wamehimizwa kujiandaa kunufaika na fursa zitakazoambatana na mradi mkubwa wa kuchataka gesi asilia uliopo kata ya Mbaja, Manispaa ya Lindi.
hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali Mkoani Lindi (LANGO), Michael Mwanga katika mkutano wa hadhara uliolenga kujenga uelewa wa wananchi kuhusu kujiandaa na fursa za mradi huo kwa kuzingatia Sera ya Ushirikishwaji wa Wazawa.
Amewataka wananchi kutambua umuhimu wa kutafuta taarifa sahihi za mradi huo katika vyombo sahihi na kuona namna wanavyoweza kushiriki katika fursa hizo na kutumia changamoto zitakazo jitokeza kama fursa ya kusonga mbele kiuchumi.
Pia amewataka wananchi kutokaa na kusubiri mradi huo uanze ndipo nao waanze ujenzi wa majengo ya kupanga, kuendesha mashamba na bustani za mbogamboga, na ufugaji wa kuku, bali watumie muda huu kufanya maandalizi ili punde mradi utakapoaanza na wao waanze kunufaika na mradi huo.
Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Lindi, Methusela Magayane akizungumza katika mkutano huo aliwataka wakazi wa Lindi kufika katika Ofisi za Halmashauri Lindi kukopa fedha ili kujiandaa na fursa zitakazoambatana na mradi huo utakaoanza hivi karibuni.