LANGO kupitia Mradi wa Kupinga ukatili wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana, limefanya zoezi la ugawaji wa vifaa vya kunawia mikono katika shule za msingi 7 na shule za sekondari 2 zilizopo katika kata za Mbanja na Mchinga wilayani Lindi ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za serikali na wadau wengine za kupambana na Virusi vya Korona.