Maamuzi hayo ya kuunda ushirika wa Mwani kata ya Mchinga yameafikiwa katika kikao kilichowakutanisha vikundi vya zamani na vikundi vipya vya wakulima wa mwani katika kata ya Mchinga Manispaa ya Lindi, kikao kililenga kubadilishana uzoefu, mafanikio, changamoto na fursa walizozipata katika vikundi hivyo ili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa zao la mwani.
Vikundi hivyo vimefikia uamuzi huo baada ya kuona faida za vyama mbalimbali vya ushirika vya wakulima wa mazao mengine kama korosho na ufuta, jinsi ushirika unavyotumika kama, miamvuli ya kuwatambulisha wakulima pamoja na kuwasogeza kwa pamoja kupata fursa mbalimbali katika kilimo.
Wameongeza kuwa ziara ya Zanzibar iliwapa chachu na ari, kwa kuona jinsi ushirika wa Furahia Wanawake Cooperative ulivyo wanufaisha wakulima wa mwani Paje, Zanzibar ikiwemo kuivutia serikali kuwapa vitendea kazi vinavyorahisisha shughuli za kikundi hiko.
Kwa sasa wanavikundi hao wa Mchinga wapo katika michakato ya awali ya kuanzisha ushir
Shirika la LANGO kwa udhamini wa shirika la Oxfam Tanzania limeratibu vikao hivyo kwa lengo la kuibua mijadala baina ya wakulima wa zao la mwani ili waweze kupanua uelewa na kuongeza uzoefu ili wana Mchinga wafanye kilimo cha mwani chenye kuleta tija.